Ucheleweshaji wa Upelelezi wa Kesi Wamchefua Rais Magufuli



Rais John Magufuli amesema bado kuna ukosefu wa maadili kwa baadhi ya Watumishi wa Idara ya Mahakama nchini, hali ambayo haimfurahishi.

Akihutubia jijini Dar es salaam katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini, Rais Magufuli amesema kuwa ukosefu huo wa maadili miongoni mwa Watumishi wa Idara ya Mahakama umekua ukisababisha Wananchi kukosa haki, kuwepo kwa idadi kubwa ya Mahabusu zaidi ya wafungwa na kucheleweshwa kusikilizwa kwa kesi mbalimbali.

"Lakini niwaombe ndugu zangu wapelelezi, kwamba ufalme wa mbinguni utakuwa shida kwenu, msipotubu na kumrudia Mungu kwa sababu roho za wasiokuwa na hatia zinaangamia kule, mnawapa shida Mahakimu na Majaji na roho za watu, nawaambia ukweli mtaenda kuyalipa badilikeni" amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa kwa sasa Magereza ina zaidi ya watu elfu 30,000, wafungwa wakiwa ni 13,455, mahabusu 17,632 hali inayoashiria uwepo wa tatizo kubwa kwa wapelelezi wa kesi hizo.

"Kuna msongamano kwenye magereza zetu, wengine kesi zao ni za kusingiziwa au wengine wako mahabusu wanateseka kwasababu ya Matajiri kusema ‘ nakukomesha utakaa mahabusu’, Wapelelezaji nao kila siku upelelezi unaendelea tena kwa makusudi msipotubu ufalme wa Mungu itakuwa vigumu kuuona”- JPM

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad