Umoja wa Nchi za Kiarabu Waukataa Mpango wa Rais Trump


Umoja wa nchi za kiarabu umepinga kwa ujumla kile kilichoitwa mpango wa amani, makubaliano ya karne ya Rais Donald Trump wa Marekani.

Umaja wa mataifa ya kiarabu ulikutana katika mkutano usio wa kawaida mji mkuu wa Misri, Cairo.

Ahmet Abul Geyt  akihutubia  wakati wa  kufunga mkutano huo alifafanua kwamba wameukataa mpango wa Trump,

“ Kinachoitwa mpango , haukidhi haki za msingi za raia wa Palestina” alisema

Naye waziri wa mambo ya nje wa Palestina  Riyad Maliki, alitanabaisha kwamba mwishoni mwa mwezi huu, Rais Mahmud Abbas wa Palestina atahudhuria mkutano wa baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa.

Rais Trump wa Marekani na waziri wa mambo ya nje wa Israel mnamo Januari 28 kwa pamoja walitangaza mpango wao wa kuigawanya Palestina.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad