Unaambiwa Aslay na Mbosso wa WCB Wasafi Paka na Paja.....

Kama ulikuwa unatarajia kolabo kati ya mafahali wengine wawili wa Bongo Fleva; Aslay Isihaka Nassoro na Mbwana Yusuph Kilungi ‘Mbosso Khan’, sahau jambo hilo kwa sasa


Aslay na Mbosso ni miongoni mwa wasanii wakali waliokuwa wakiunda Kundi la Yamoto Band ambalo lilikuwa gumzo ndani na nje ya Bongo kabla ya kuvunjika yapata miaka mitano iliyopita na sasa kila mmoja anapambana kivyake.

Wengine waliokuwa nao Yamoto Band ni Beka Flavour na Enock Bella chini ya Said Fela ‘Mkubwa na Wanawe’.

amaa hao wapo kwenye mtifuano mzito kwa muda mrefu tangu waliposambaratika.

Mara baada ya kusambaratika, Aslay ndiye aliyekuwa wa kwanza kuachia nyimbo zake binafsi ambapo Mbosso aliamua kurejea kijijini kwao mkoani Pwani.

Kufuatia Aslay kuachia nyimbo mfululizo, baadaye yalisikika madai kutoka kwa wenzake hao kuwa, yeye (Aslay) ndiye chanzo cha kuvunjika kwa Yamoto Band, madai ambayo huwa hataki kuyajibu.

MBOSSO WASAFI, ASLAY AMPOTEZEA

Ilidaiwa kuwa, kabla ya kujiunga na Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) chini ya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Mbosso alikuwa akilalamika kuwa kila alipompigia simu Aslay alikuwa akimpotezea.

Lakini baada ya Mbosso kuchukuliwa na Wasafi, ndipo hali ilipozidi kuwa mbaya juu ya uhusiano wao na sasa hata simu wakawa hawapigiani.
WIVU WATAJWA

Mara tu baada ya Mbosso kusainiwa na Wasafi, kumekuwa na tetesi za kuoneana wivu na kufikia hatua ya kushindanishwa wenyewe kwa wenyewe

“Mimi ninauheshimu muziki wa Aslay kwa sababu ni mtu ambaye nimemkuta kwenye industry, halafu kwangu mimi yule ni brother.”

Hata hivyo, mashabiki wao wamekuwa wakitofautiana, huku kila upande ukiamini msanii wake ni mkali kuliko mwingine.

KUJIMWAMBAFAI

Katika hali kama hiyo, hata wao wenyewe (Aslay na Mbosso), kila mmoja anadaiwa kujimwambafai na kujiona yupo juu kuliko mwenzake.

“Wale hawawezi kuelewana kwa sababu kila mmoja anajiona yupo juu kuliko mwenzake.

“Siyo vibaya mtu kujiamini sana, ushindani unaleta chachu kwenye gemu la Bongo Fleva.

“Mimi sioni kama mabifu yana ubaya kama lengo ni kushindana kimuziki, lakini wasijengeane chuki,” alisema mwigizaji wa Bongo Movies ambaye pia anafanya Bongo Fleva, Laurent Ngubilu.

“Nilimsapoti sana (Aslay) kwa muda mrefu, lakini nilionekana ninajipendekeza,” alisema Mbosso alipoulizwa na gazeti hili juu ya uhusiano wake na Aslay na kuongeza;

“Baada ya kumsapoti Aslay kwa muda mrefu, watu wakawa wananiambia mbona wewe unamsapoti halafu yeye hakusapoti?

“Mtu umem-follow (kwenye Instagram), mwenzako ameku-unfollow. Jifunze kubalansi shobo, nikasema kumbe na mimi naonekana namshobokea… ngoja na mimi nim-unfollow.

“Kwa hiyo nisiwe mnafiki, kwa sasa hivi kila mtu hana urafiki na mwenzake.”

HUYU HAPA ASLAY

Kwa upande wake Aslay alipoulizwa hivi karibuni juu ya uhusiano wake na Mbosso alikuwa na haya ya kusema;

“Kuna matatizo ambayo siwezi kuongea kwani mwisho wa siku kila kitu kinaendea freshi, tusiendelee tena kuleta kitu kingine.”

Alipoulizwa kama ana mpango wa kufanya kolabo na Mbosso, Aslay alisema hana la kusema.

BEKA VITA NA ASLAY

Ukimwacha Mbosso, msanii wa Yamoto, Beka Flavour naye anatajwa kutoivana na Aslay.

Katika maelezo yake, Beka alikanusha maelezo kuwa anamwogopa Aslay kutokana na kipaji chake kikubwa.

“Hakuna kitu kama hicho, wale wenye fikra kuwa ninamuogopa waendelee kufikiria hivyo, muziki wangu sija-focus kwake, nime-focus kwa watu wakubwa wengine,” alisema Beka akieleza uhusiano wake na Aslay.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad