Unaambiwa TSH Bilion 12 Zapatikana Kwa Makosa ya Uhujumu Uchumi..



Wakati takriban Sh bilioni 12 zikipatikana kutokana na watuhumiwa wa makosa ya Uhujumu Uchumi, zaidi ya Sh bilioni 19 zimepatikana baada ya kutaifisha mali mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema fedha hizo kutoka kwa wahujumu uchumi zilipatikana baada ya watuhumiwa kuomba radhi na kurejesha kiasi hicho cha fedha walichoshtakiwa kuhujumu

Pia alikabidhi mali zilizotaifishwa yakiwemo magari, fedha taslimu, dhahabu na nyumba zilizopo maeneo mbalimbali nchini

Mali zilizokabidhiwa ni madini ya Dhahabu kilo 46.177 yaliyokuwa na thamani ya zaidi ya Sh bilioni tatu, madini ya Almasi, Tanzanite, Bati, Saphire na madini mengine sambamba na nyumba 24 zilizotaifishwa, magari 65, mashine ya kubaini ubora wa kemikali mbalimbali na madini pamoja na viwanja na mashamba

SOMA HABARI HIZI KIRAHISI KUPITIA APP YETU YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD HAPA

Hata hivyo, alisema thamani ya jumla kuu ya mali zilizotaifishwa na kukabidhiwa kwa Benki Kuu ya Tanzania kwa ajili ya kuhifadhiwa na zile ambazo zipo tayari kwenye akaunti maalumu ni zaidi ya Sh bilioni 58.6
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad