Usiyoyajua Kuhusu Majimaji Ukeni
0
February 08, 2020
Uchafu unaotoka katika sehemu za siri za mwanamke au kwa msamiati wa Kiswahili ‘mchozo’ ambao si wakawaida, huo ni ugonjwa.
Kwa kawaida uke hutoa maji maji yenye rangi ya maziwa ambayo huwa myembamba na meupe na huwa hayana harufu yakukera, kuchoma au mwasho au kuambatana na vipele.
Kiwango chake pamoja na muonekano wake kwa siku unaweza kubadilika kadiri umri unavyopiga hatua. Kutokana na maelezo yako, ina maana ute huo si wa kawaida, kwani ni mzito.
Dalili hiyo ni ya fangasi za ukeni, inaweza kuwa na mwonekano kama vile maziwa ya mgando inaweza kuwa na muwasho.
Tatizo hili linatibiwa kwa dawa za fangasi za kutumbukiza kwenye sehemu za siri. Nakushauri fika katika huduma za afya zilizo jirani kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hilo.
Zipo sababu mbalimbali zinazoweza kusababisha uchafu huo ikiwamo uwapo wa vitu vigeni ukeni kama vipande vya pedi au pamba, uambukizi wa bakteria, parasite, fangasi na virusi.
Uchafu unaotokana na uambukizi wa bakteria huwa na harufu kama shombo la samaki ambayo huisiwa baada ya kujamiana na unaweza kuwa na rangi ya kijivu, kijani kibichi njano au mchanganyiko na damu.
Kama ni maambukizi ya fangasi ni kama nilivyoeleza katika swali la kwanza, uambukizi wa parasite uchafu unaotoka huwa ni mwingi na unakuwa na harufu mbaya, wenye rangi kijani au njano na wenye povu.
Pia uambukizi wa bakteria unaweza kuambatana na utokaji wa usaha, vipele au vidonda na muwasho.
Kumbuka magonjwa hayo yanahitajika kutibiwa na wenza wote wawili mnaoshirikiana tendo la ndoa ili kuepuka tatizo kujirudia.
Katika kipindi cha matibabu, tendo la ndoa lazima liwekwe kando kwanza, mpaka atakapopona.
Tags