Uswisi yaunga mkono marufuku dhidi ya ubaguzi wa mashoga


Uswisi wamepiga kura jana Jumapili kupiga marufuku ubaguzi wenye misingi ya mwelekeo wa uamuzi wa mtu katika tendo la ngono.

Kura ya maoni nchini humo inayochukua misingi ya demokrasia inabeba masuala kadhaa yanayoleta mtengano kwa umma iwapo watu wengi watapendelea.

Kura ya maoni ya jana Jumapili iliamua kuhusu sheria ambayo hususan inapiga marufuku matamshi ya chuki na ubaguzi kwa misingi ya mwelekeo wa mtu kufanya ngono ambapo adhabu ni kifungo cha jela cha hadi miaka mitatu.

Sheria ya jinai kwa hivi sasa inajumuisha ubaguzi kwa misingi ya rangi, kabila na dini. Kiasi ya asilimia 60 ya wapiga kura wamekubaliana na sheria hiyo, ambapo vyama vingi vimeunga mkono mabadiliko hayo ya kuwalinda mashoga, na jamii ya wanaofanya mapenzi kwa jinsia moja.

Hata hivyo , chama cha siasa za mrengo wa kulia cha Swiss People's Party SVP, chama kikubwa bungeni , kinapinga sheria hiyo.

 Chama cha SVP kinadai kuwa wahamiaji wameingiza mawazo ya chuki dhidi ya wageni na kwamba mdahalo wa jamii na kufukuzwa kwa wachochezi wa kigeni utakuwa bora zaidi.

 Mabadiliko hayo yalipitishwa kwanza na bunge la Uswisi mwaka 2018, lakini yalilazimika kupita katika kura ya maoni baada ya wakosoaji kusema yatavuruga uhuru wa kutoa maoni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad