VIDEO: Nabii Mwamposa Adaiwa Kukaidi Kibali Alichopewa na Polisi Kuendesha Mkutano wa Moshi Ulioua Watu


Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi George Simbachawene amesema Nabii na Mtume, Boniphace Mwamposa alikaidi taratibu za kibali kilichomtaka afanye huduma mpaka saa 12 jioni, huduma aliyoitoa hadi saa 2 usiku na kuwaamuru waumini wakanyage mafuta kabla ya maafa hayo kutokea.

Simbachawene ameyasema hayo Jijini Dodoma leo Jumapili Februari 2, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema baada ya Mwamposa kuona maafa hayo yametokea, alitoroka ili kukwepa polisi na kurudi jijini Dar es Salaam usiku huohuo.

“Askofu (Nabii na Mtume) Mwamposa alipewa kibali cha kufanya huduma hiyo hadi saa 12 jioni lakini yeye hakutii, badala yake aliendelea na huduma na ilipofika saa moja jioni hadi saa mbili usiku yakatokea maafa hayo ya watu wakati wa kukanyaka mafuta hayo,” amesema Simbachawene.

Amesema mbali na Mwamposa kukamatwa wapo watu wengine  waliokamatwa Moshi kutokana na tukio hilo akiwamo Mchungaji Elia Mwambamba ambaye ndiye aliyeomba kibali cha mkusanyiko huo.


Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilia.

Aidha, Simbachawene amesema Mwamposa amekamatwa na polisi leo alfajiri Jijini Dar es Salaam baada ya kutoka Moshi, Mkoani Kilimanjaro.


"Mwamposa alimwaga mafuta ya upako kwenye turubai ili watu wakayanyage, lakini baada ya kuona maafa hayo yametokea akatoroka hadi Dar es salaam lakini tukafanikiwa kumkamata na tunafanya utaratibu wa kumpeleka Moshi ili kukabiliana na tuhuma zinazomkabili," amesema Simbachawene.

Hata hivyo, wakati Waziri Simbachawene akisema Nabii Mwamposa ametiwa mikononi mwa polisi leo alfajiri, kiongozi huyo wa dini alionekana Kanisani kwake Kawe asubuhi alikoongoza ibada na baadaye saa 4:30 aliwaaga waumini wake kuwa anaelekea Moshi mkoani Kilimanjaro kuitikia wito wa polisi.

VIDEO:

By Nazael Mkiramweni, Mwananchi. nmkiramweni@mwananchi.co.tz
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Simbachawene, Kongole mwaha...!!
    karibu kazini.

    Mwapoasiyo Mtume wala Nabii..

    Nimejaribu kupata Tafsiri haziendani.

    SADC countries wamekubali kutumia lugha yetu. Naomba tuitumie vyema.

    ReplyDelete
  2. Simbachawene, Kongole mwaha...!!
    karibu kazini.

    Mwamposa siyo Mtume wala Nabii..

    Nimejaribu kupata Tafsiri haziendani.

    SADC countries wamekubali kutumia lugha yetu. Naomba tuitumie vyema.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad