Waasi wadungua ndege ya kivita ya Saudi Arabia nchini Yemen



Ndege ya kivita ya Saudia Arabia, jeshi linalopambana nchini Yemen imeanguka katika jimbo la kaskazini al-Jawf.

Msemaji wa jeshi amethibitisha kuwa ndege ya kivita ya Saudia ''imeanguka'' ikiwa imebeba vifaa kwa ajili ya kusaidia operesheni ya kijeshi karibu na kambi ya jeshi la Yemen, kwa mujibu wa shirika la habari la Saudi Arabia, SPA.

Waasi wa houthi wamesema wameidungua ndege hiyo Ijumaa usiku.

Umoja wa Mataifa umesema raia 31 waliuawa katika shambulio la anga jimboni al-Jawf siku ya Jumamosi.

Majeshi ya muungano yanayoongozwa na Saudi Arabia yamekuwa yakipambana na waasi wa kihuthi tangu mwaka 2015. Iliingilia kati baada ya waasi kuindoa madarakani serikali inayotambulika na jumuia ya kimataifa, mjini Sanaa.

Waasi wa houthi wamesema walitumia makombora kuiangusha ndege ya kijeshi usiku wa siku ya Ijumaa.

Saudi Arabia haijatoa taarifa zaidi kuhusu athari kutokana na kuanguka kwa ndege yake wala sababu za kuanguka kwa ndege hiyo.

Imesema imefanya operesheni ya utafutaji na uokoaji siku ya Jumamosi na kuwa baadhi ya raia huenda wameuawa bila kukusudiwa.

Maafisa wa Kihouthi wamesema watoto ni miongoni mwa waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya anga dhidi ya Saudi Arabia, ambayo wamesema ni kulipiza kisasi kwa kile walichodai kuwa majeshi hayo yalikuwa yakiwalenga raia kwenye maeneo ambayo waasi waliangusha ndege hiyo.

Wamesema kuwa baadhi ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.

Katika taarifa yao mratibu wa masuala ya kibinaadamu wa UN nchini Yemen Lise Grande ametoa ''salamu za rambirambi kwa familia za waliouawa.''

Yemen imekuwa katika vita tangu 2015, wakati rais Abdrabbuh Mansour Hadi na baraza lake la mawaziri lilipolazimishwa na waasi wa Houthi kuondoka mji mkuu Sanaa - ambao wanadhibiti sehemu kubwa za eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.

Saudi Arabia inamuunga mkono rais Hadi, na imeongoza muungano wa mataifa ya kieneo katika mashambulio dhidi ya waasi hao wanaungwa mkono na Iran.

Muungano huo hufyatua makombora karibu kila siku, wakati waasi wa Houthi hurusha makombora dhidi ya Saudia.

Vita hivyo vimesababisha vifo vya raia na janga baya duniani la kibinaadamu, huku asilimia 80 ya idadi ya watu - ambayo ni zaidi ya watu milioni 24 - wakihitaji usaidizi wa kibinaadamu au ulinzi, pamoja na watu milioni 10 wanaotegemea chakula cha misaada ili kuendelea kuishi.

Zaidi ya watu 70,000 wanaaminika kufariki tangu 2016 kutokana na mzozo huo, Umoja wa mataifa unakadiria.
OPEN IN BROWSER
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad