Wabunge Waitaka Serikali Kutong'ang'ania Maiti Ndugu Wanaposhindwa Kulipia Gharama za Matibabu



Wabunge wametaka Serikali kuacha tabia ya kushikilia miili ya wanaofariki na ndugu zao kushindwa kulipa gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaofariki badala yake iwasamehe

Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Mussa Mbarouk wa Tanga wameyasema hayo wakati wakichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii

Sugu amesema Serikali imekuwa ikisema hakuna Mtanzania anayekosa matibabu lakini wanashikilia maiti hospitalini na hatua hii inawanyima Watanzania kwenda kufanya ibada kwa ndugu zao wanaofariki kwa kushindwa kulipia gharama za matibabu

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Faustine Ndugulile amejibu hoja hiyo kwa kusema Wananchi wanaokosa fedha za kulipia matitabu wanapaswa kwenda kwenye Dawati la Ustawi wa Jamii linalokuwepo katika kila Hospitali

Aidha, ameongeza kuwa hawana maiti ambayo wanaishikilia kwasababu ya madai ya gharama za matibabu kutokana na kuwepo kwa Dawati hilo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad