Wakala wa Pogba uso kwa uso na Solskjaer baada ya majibizano makali, wengine sokoni Jumatano hii



Bongo5 · Hamza Fumo · 5 hours ago
Wakala wa Pogba, Mino Raiola anasema kuwa ana mpango wa “kuwasiliana” na mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer baada ya majibizano makali kumhusu mteja wake. (Sky Sports)



Ndugu wa Pogba wa kiume Mathias anasema kuwa “kila mtu anajua” kwamba anataka kuondoka Manchester United “kwenda kucheza soka ya Champions League na kushinda mataji”. (Sun)

Ole Gunnar Solskjaer alishindwa kuvumilia vitimbi vya wakala wa Kiungo fundi wa United na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba na kusema kuwa hatma ya nyota huyo ipo mikononi mwa Manchester na sio kwa Mino Raiola.

Wakala wa Pogba, Mino Raiola mara kadhaa amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kumtoa nyota huyo ndani ya Old Trafford, na kumpeleka katika klabu nyingine.

Pengine Mino Raiola akikutana Ole Gunnar Solskjaer wanaweza kumaliza tofauti zao, na kumuacha kijana kuendelea kuitumikia United kwa kuwa bado anamkataba na Manchester

Kiungo wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba anatarajiwa kuondoka Manchester United msimu huu lakini klabu hiyo inataka zaidi ya paundi milioni 150 kumuachilia mchezaji huyo wa miaka 26. (ESPN)

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard atakuwa kwenye wakati mgumu kama endapo klabu hiyo itashindwa  Champions League msimu huu. (Telegraph)Frank Lampard

Mkufunzi wa Chelsea Frank Lampard atajikuta mashakani ikiwa haitafuzu kwa Champions League

Manchester City inamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry, 24, kama sehemu ya mpango utakaomwezesha Leroy Sane, 24, kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga. (Sun)

Manchester United wanatafakari uwezekano wa kuwasajili mkurugenzi wa zamani wa michezo Paris St-Germain Antero Henrique na mkuu wa michezo wa Red Bull Ralf Rangnick katiki wadhifa wa mkurugenzi wa kiufundi. (Independent)

Beki wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, 21, amesema anajua kuwa ”ananyatiwa” na Barcelona na Arsenal. (RMC Sport, via Goal)Leroy Sane

Manchester City inamtaka winga wa Bayern Munich Serge Gnabry kubadilishana nafasi na Leroy Sane (Kulia)

Chelsea inamtafuta kiungo wa kati wa Birmingham City mwenye umri wa miaka 16 Jude Bellingham, lakini Manchester United, Barcelona na Real Madrid pia zimeonesha nia yakumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza wa chini ya miaka -17. (Goal)

Barcelona inamlenga mshambuliaji wa Denmark na Leganes Martin Braithwaite, 28, baada ya kupewa ishara ya kumtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, baada ya kusitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Real Sociedad Mrazil Willian Jose, 28. (Sky Sports)

Manchester City huenda ikakabiliwa na uchunguzi zaidi kutoka Uefa ili kubaini kiwango cha wafadhili wake wa Abu Dhabi baaada ya kuwekewa marufuku ya kushiriki mashindano ya ulaya baada ya kupatikana na kosa la kiuka sheria ya uchezaji haki kifedha. (Guardian)


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad