Wakurugenzi 10 Kupelekwa Kwa JPM


Waziri wa TAMISEMI, Seleman Jafo, amewaagiza Wakuu wa Idara za Fedha katika halmashauri 10 zilizofanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato kujitathimini nafasi zao hadi ifikapo Juni 30 mwaka huu.


Waziri Jafo ameyasema hayo leo, Februari 9 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo ameagiza wajitathmini hadi Juni 30 vinginevyo nafasi zao watapewa watu wengine.

"Wakurugenzi wa halmashauri ambazo zimesuasua katika ukusanyaji mapato, majina yao nitayapeleka kwa mwenye mamlaka husika ili waangaliwe Kama wanafaa kwenye nafasi zao", amesema Mh. Jafo.

Mhe. Jafo amesema Serikali inatilia mkazo suala la ukusanyaji mapato, hivyo haitawavumilia maafisa wanaolegalega kwenye suala hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad