Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya DSM,Lazaro Mambosasa, amesema kuwa wanawashikilia watu wanne waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi ya G4S kwa tuhuma za kuiba Sh1.2 bilioni, dola za Kimarekani 402,000 pamoja na Euro 27,700.
Akitoa taarifa hiyo leo Februari 25, 2020, Kamanda Mambosasa amesema walinzi hao walikabidhiwa fedha kutoka tawi la NBC kariakoo na Samora ili wazipeleke makao makuu ya Bank hiyo Posta ya zamani, Sokoine Drive, badala yake wakatokomea nazo hadi maeneo ya Temeke Maduka mawili na kuiba fedha zote.
"Jeshi la Polisi kanda maalum limefanikiwa kukamata watuhumiwa wote watatu, pamoja na mtuhumiwa mmoja ambaye aliwasaidia kukamilisha wizi huo, pia tunawashikilia Askari Polisi Tisa kwa kukiuka maadili ya kazi wakati wa ufutiliaji na upekuzi wa tukio hili" amesema Kamanda Mambosasa
Waliokamatwa ni Christopher Rugemalila, Mohamed Ramadhan, Ibrahim Maunga, pamoja na Salum Shamte.