Wanajeshi wavamia Bunge kushinikiza muswada kupitishwa


Wanajeshi na maafisa wa polisi waliojihami nchini El Salvador wamevamia bunge, wakitaka kuidhinishwa kwa muswada wa kuruhusu mkopo wa dola milioni 109 ili kuwanunulia vifaa vya kukabiliana na uhalifu.

Waliingia katika jengo la bunge wakati rais wa nchi hiyo, Nayib Bukele alipokuwa anakaribia kuwahutubia wabunge .

imeelezwa kuwa, Viongozi wa upinzani walitaja uvamizi huo wa wanajeshi bungeni kuwa kama kitendo cha kutishia.

Rais Bukele ambaye alichukua mamlaka mwezi Juni 2019, anataka kutumia mkopo huo kuimarisha vifaa vya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vita dhidi ya uhalifu.

Sababu 5 zisizoepukika mtoto mchanga kulialia usiku
Ameahidi kukabiliana na ghasia zinazotekelezwa na wahalifu pamoja na ufisadi katika taifa hilo lenye viwango vya juu vya umasikini.

Siku ya Jumapili, mamia ya watu walikongamana nje ya bunge katika mji mkuu wa San Salvador kuunga mkono mpango wa usalama wa rais.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad