Wanazuoni wa CCM Mkoa wa Kigoma Watoa Tamko Dhidi ya Zitto Kabwe



FAMILIA ya wasomi wa Chama cha mapinduzi(CCM) mkoani kigoma wanazuoni wametoa tamko juu ya kitendo alichokifanya mbunge wa kigoma mjini mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe cha kupeleka maombi ya zuio la mkopo kwa serikali ya Tanzania bank kuu kwaajili ya kuboresha Elimu.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Mkoa za chama cha mapinduzi wanazuoni hao wamesema kuwa jambo alilolifanya Zitto halikubaliki na ni kitendo kisichoungwa mkono kabisa na wanakigoma na hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.

"Kitendo alichokifanya Zitto siyo kitendo kizuri kwasababu Zitto ni mbunge kwani ana uwanja mkubwa wa kuzungumza hayo bungeni nasiyo kuandika barua binafsi yeye kama zitto ya kuzuia fedha za mkopo wa kuboresha elimu toka bank kuu"alisema Eliya Michael mwana CCM na mwanazuoni wa Mkoa wa Kigoma

Eliya alisema kuwa Zitto anapaswa kukemewa kwa jambo alilolifanya kukaa kimya watu wataona jambo alilolifanya ni sahihi lakini wao kama wanakigoma wanasema alichokifanya zitto hakipaswi kuigwa na mtu yeyote.

Naye William Mtula mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa alisema kuwa hivi sasa ni wakati wa watanzania kuungana pamoja na kumtia moyo Rais kwa kazi kubwa na nzuri anazozifanya za kuwaletea maendeleo wananchi.

Mtula alisema kuwa matakwa ya Watanzania nikupata huduma bora na za msingi kama vile elimu,afya,miundombinu na zingine.

"Zitto ni mbunge pia ni mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kigoma mjini bungeni hivyo alipaswa kuongelea hoja za wananchi wake na kero zilizopo jimboni kwake na sihayo aliyoyafanya dhidi ya serikali yake"alisema

Wanazuoni hao wamewataka wananchi wa jimbo la Kigoma mjini kulitafakari hilo na kuona sasa ni wakati wao wa kutafuta mwakilishi ambaye atawawakilisha vizuri na siyo yule anayefanya kazi amabazo wananchi hawajamtuma.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad