Watanzania Tumsaidie Mbwana Samatta....



WATANZANIA wamegeuza mitandao ya kijamii ya klabu ya Aston Villa ya England kama sehemu ya kijiwe cha kutukana na kuwakejeli wachezaji, ambao wanahisi hawaoneshi ushirikiano kwa nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye ni tegemeo lao kwa sasa.

Watanzania wanaonekana wanapenda kuona Samatta anafanikiwa kuliko Villa wenyewe ambao walitoa kitita cha fedha cha pauni milioni 8.5 kumsajili kutoka KRC Genk ya Ubelgiji wakihitaji huduma yake kwenda kutibu tatizo kwenye safu ya ushambuliaji.

SHAUKU YA WATANZANIA

Watanzania hamu yao ni kuona kila mchezo Samatta anafunga mabao na kung’ara kwenye ligi hiyo pendwa inayotazamwa na watu wengi duniani kote, wakiwemo wale wanaoiangalia kupitia vibanda umiza. Inawezekana kwa sasa maofisa wa Villa wanafikiria namna ya kutafuta mkalimani wa kutafsiri kutokana na mitandao yao kuwa bize muda wote kupokea jumbe kwa lugha ya Kiswahili.

SAMATTA AIBUKA

Samatta mwenyewe mwishoni mwa wiki iliyopita alilazimika kutoka hadharani kuwaomba Watanzania waache tabia ya kutukana kwenye akaunti za timu hiyo na zile za wachezaji akihofia huenda wakamsababishia uhusiano mbaya na wachezaji wenzake wapya ndani ya uwanja. Watanzania wameanza kugeuza mitandao ya instagram ya Villa kama kijiwe cha kuonesha makali yao kwa kuwatunishia misuli wachezaji wa timu hiyo wanaoonekana kumtibulia Samatta mipango ya kupachika mabao.

Hali hiyo inamkuta Samatta anayetazamwa na watanzania kama kioo kwa sasa kulingana na mafanikio aliyofikia ikiwa ni baada ya kucheza michezo miwili dhidi ya Leicester City ambao Villa walishinda mabao 2-1 mechi ya nusu fainali ya Kombe la Carabao na ule wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth FC ambao hata hivyo Villa walipoteza kwa mabao 2-1, lakini Samatta akipachika bao la kufutia machozi.

Samatta anasema yeye binafsi hafurahishwi na hali hiyo inayoendelea ingawa anafahamu mashabiki wanapenda afanye vizuri kwenye timu hiyo, lakini anawaomba waache na kama wataendelea wanaweza kumtengenezea mazingira magumu na wachezaji wenzake.

“Mashabiki wa soka Tanzania nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye malengo mabaya na timu au wachezaji binafsi sifurahishwi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad