Watoto Wanavyosumbua Vichwa vya Mastaa



KUNA usemi usemao kuwa mtoto si nguo utaomba mtu, ndivyo ilivyo kwa baadhi ya mastaa mbalimbali hapa nchini ambao wamebarikiwa kupata umaarufu mkubwa lakini bado ndani ya mioyo yao furaha yao haijakamilika kwa sababu hawajabahatika kupata watoto. 

 

Kwenye mitandao mingi ya kijamii, mastaa wamekuwa wakionyesha furaha zao kwa kuwa na watoto na hata kwenda kupiga nao picha na kuzitupia kwenye mitandao hiyo, kutoka nao sehemu mbalimbali kitu ambacho kinakuwa kama miiba kwa ambao hawaja-jaaliwa kupata watoto. Katika makala haya, nakuletea baadhi ya mastaa ambao ni maarufu lakini hawajapewa uzao.

 



WEMA SEPETU

Huyu ni staa mwenye jina kubwa na amejizolea umaarufu mkubwa akiwa Miss Tanzania 2006, mwigizaji na sasa mjasiriamali.

 

Lakini kikwazo cha utimilifu wa furaha kimekuwa ni kukosa mtoto, kitu ambacho kila siku kimekuwa kinamuumiza mrembo huyo. Mara kadhaa amekuwa akiilazimisha furaha ya kuwa na mtoto kwa kutupia picha mbalimbali za watoto wa wenzake na kueleza hisia za maumivu ya moyo anayokabiliana nayo.

 

Mara nyingi staa huyo amekuwa akiweka wazi kuhusu kuasili mtoto kwa kuhisi hawezi tena kupata mtoto kwenye umri alionao. Ikiwa sababu za kukwama kupata mtoto hazijawekwa wazi na alipoishia ni kuwafanya watoto wa marafiki zake kuwa kama wake ili siku za maisha yake zisogee.

 



JACQUELINE WOLPER

Ni msanii maarufu wa Filamu nchini, lakini naye hajabahatika kupata mtoto, mara nyingi amekuwa akiumia ndani kwa ndani na hata kuwaeleza watu wake wa karibu juu ya kutamani kupata mtoto kama walivyo mastaa wengine.

 

Wolper amedai hana shida kwenye mfumo wa mwili wake kuhusu kutopata mtoto, ila sababu kubwa ni kwamba hajapata baba ambaye anaweza kuzaa naye mtoto na akamtunza ipasavyo.



JACOB STIVEN ‘JB’

Huyu ni msanii wa kitambo kwenye anga la filamu, ni maarufu mkubwa lakini naye kama walivyo kina Wema na Wolper, hana mtoto. Binafsi yake mara nyingi amekuwa akikwepa kuongelea ‘ugumba’ wake akiwa na imani kubwa kwa Mungu kuwa ipo siku ataitwa ‘baba’.



REHEMA CHALAMILA ‘RAY C’

Enzi zake alijulikana kama ‘kiuno bila mfupa’ kwa jinsi alivyokuwa akikizungusha jukwaani kwenye shoo zake huku wimbo wake wa Uko Wapi ukimpa kiki ya kutosha.

 

Amekuwa maarufu kwenye sanaa ya muziki na baadaye kutopea kwenye madawa ya kulevya kabla ya kuyaacha na kuolewa na Mzungu, lakini ishu imebaki kuwa ‘hana mtoto’ mpaka sasa.

 

Jambo hili limekuwa likimuumiza sana msanii huyo kiasi cha kuwaambia rafiki zake kuwa ana kiu ya kuitwa ‘mama’ lakini ndiyo hivyo mambo hayajakaa sawa.



LADY JAY DEE

Jina lake kamili ni Judith Wambura hilo lililopo hapo juu ni a.k.a yake, lakini ni msanii maarufu nchini ambaye amewahi kutamba na wimbo wa Machozi ya Furaha.

 

Pamoja na mafanikio yake kimuziki, kikwazo cha furaha ya msanii huyo kimekuwa ni kukosa mtoto jambo ambalo mara kadhaa amekuwa akikiri kuwa linamtesa huku sababu za kutopata mtoto zikibaki sirini kwa Mwenyezi Mungu.

Stori: Neema Adrian, Uwazi


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad