Watu Wenye Umri Mrefu Duniani Wapatikana Japan
0
February 13, 2020
Mtandao maarufu wa kutunza rekodi duniani "Guiness World Records" umemtaja na kumkabidhi cheti bwana Chitetsu Watanabe kutoka Niigata Japan, kama ndiyo mwanaume mwenye umri mrefu zaidi duniani akiwa na miaka 112.
Bibi Kane Tanaka na Babu Chitetsu Watanabe, waliovunja rekodi ya kuwa na umri mrefu zaidi Japan
Babu huyo Chitetsu Watanabe ni mtoto wa kwanza kati ya watoto 8 kutoka kwa Baba yake na Mama yake na amezaliwa Machi 5, 1907.
Kwa mujibu wa mtandao huo umempongeza mzee huyo kuwa mwanaume mwenye umri mrefu duniani kwa sasa, mwenyewe amesema siri iliyomfanya kufikia umri huo ni kutokuwa na hasira bali kuendelea kuwa na tabasamu usoni mwake.
Historia yake inaonesha mzee huyo alikuwa ni mwanajeshi na amepigana vita ya mwaka 1944, kisha akaastaafu na sasa anajishughulisha na kilimo.
Aidha kutokea hukohuko nchini Japan bibi wa miaka 117 Kane Tanaka, amekabidhiwa cheti kutoka mtandao huo wa rekodi kwa kuwa mwanamke mwenye umri mrefu zaidi duniani.
Tags