Wazazi Wapewa Siri Kuwahisha Watoto Madarasa ya Awali


Morogoro. Wakati Manispaa ya Morogoro nchini Tanzania ikiandikisha jumla ya wanafunzi 18,396 wa shule ya msingi na awali kwa mwaka 2020, wazazi wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuwapeleka mapema watoto shule za awali ili kuwajengea misingi ya maarifa.

Akizungumza na Mwananchi mjini hapa leo Jumapili Februari 23, 2020, Mwalimu mkuu wa kituo cha Tushikamane Education Centre Azimio, Manispaa ya Morogoro, Erickson Elizeus amesema kuna umuhimu mkubwa kwa mtoto wa miaka mitatu kuanza masomo ya awali ili kurahisisha uelewa wake na kumjengea maarifa.

Erickson amesema elimu bora huanzia shule ya awali na sio msingi, sekondari au chuo kwa sababu misingi bora na maarifa huanzia shule ya awali.

Amesema mtoto huanza kufundishwa stadi zote tatu za kiwango cha awali darasa shule za awali kwa kupata stadi za kuandika, kuhesabu na kusoma.

“Stadi za kuandika, kuhesabu na kusoma kwa mtoto hasa akianza kuzipata shule ya awali itamsaidia mtoto kupata mwanga mkubwa darasa la kwanza kwani ndiko tunakowajengea misingi imara ya elimu,” amesema Erickson.

Mwalimu wa darasa la kwanza shule ya msingi Mwere A, Asia Kibiki anasema  mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyepitia darasa la awali, tayari anakuwa na mwanga wa kujifunza tofauti na mwanafunzi ambaye hajasoma darasa hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad