Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, amesema wamemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kamati yake ya usalama awasamehe waongoza watalii (tour guides) waliosambaza taarifa ambazo zingeathiri biashara ya utalii Ngorongoro.
“Onyo linatosha ni vema taarifa za changamoto zikafikishwa kwetu kwa njia sahihi,” aliandika waziri Kigwangalla katika ukurasa wake wa Twitter.
Aliandika ujumbe huu ” Tumemuomba Mkuu wa Mkoa wa Arusha, mhe Mrisho Gambo na kamati yake ya usalama awasamehe tour guides waliosambaza taarifa ambazo zingeathiri biashara ya utalii Ngorongoro. Onyo linatosha. Ni vema taarifa za changamoto zikafikishwa kwetu kwa njia sahihi,”
Tumemuomba Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA, Mhe. Mrisho Gambo, na kamati yake ya usalama, awasamehe tour guides waliosambaza taarifa ambazo zingeathiri biashara ya utalii NGORONGORO. Onyo linatosha. Ni vema taarifa za changamoto zikafikishwa kwetu kwa njia sahihi #MzeeWaField #HK pic.twitter.com/jqdL60JsJZ— Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) February 22, 2020