Kigwangala ameipongeza wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuteuliwa na kuaminiwa na Raisi Magufuli katika kusimamia bodi hiyo ambayo imepewa jukumu la kusimimia Tanapa kwa kipindi kingine cha miaka 3 baada ya kufanya vizuri.
Ameitaka bodi hiyo kuja na mikakati ya kuongeza idadi ya watalii wa nje na watalii wa ndani pamoja na kuhakikisha utalii wa endelevu na shirikishi kwa jamii zinazozunguka hifadhi.
Aidha ameitaka bodi hiyo kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi ili kuhakikisha kunakua na utalii endelevu ambao ni matunda ya ushirikishwaji wa jamii zinazozunguka hifadhi
Pia ameagiza bodi hiyo kuhakikisha zoezi la uwekaji wa mipaka katika hifadhi unafanyika ili kulinda maeneo ya hifadhi yasivamiwe na kuathiri shughuli za uhifadhi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu bodi hiyo ilifanikiwa kuanzisha jeshi usu,kupambana na ujangili pamoja na kusimamia uhifadhi endelevu kwa maslahi ya taifa.
Kamishna wa Uhifadhi Tanapa ,Dr.Allan Kijazi amesema kuwa wataendelea kushirikiana na bodi hiyo katika kuimarisha na kuendeleza utendaji kazi bora wa Tanapa na hifadhi zilizoko chini yake pamoja na kuongeza mapato yanayotokana na utalii.
OPEN IN BROWSER