Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amefanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani, Umoja wa Ulaya (EU), Angola na Kuwait nchini, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo salama, na pia katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa wa huru na haki.
Akizungumza na mabalozi hao waliofika kwa wakati tofauti ofisi ndogo ya Wizara, jijini DSM, leo, Simbachawene amesema vyombo vyake vinaendelea kufanya kazi kwa weledi katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao nchini.
“Tunatarajia kufanya uchaguzi mwaka huu, na swali lako hali ya usalama nchini, tunawahakikishia nchi ipo salama, ulinzi utaimarishwa na uchaguzi utakua wa huru na haki,” Simbachawene.
Pia Waziri Simbachawene aliwahakikishia shirikiano zaidi kati ya Wizara yake na mabalozi hao katika masuala mbalimbali ya utendaji kazi.
“Tanzania itaendelea kuwa salama kwa kuwa Wizara yangu imejipanga vizuri kuendelea kuwalinda raia na mali zao pamoja na wageni wote waishio hapa nchini,” Simbachawene
Simbachawene aliwashuru mabalozi hao kwa kumtembelea, na aliwataka wawe huru muda wowote wanapohitaji kumuona wanakaribishwa ofisini kwake.
“Najisikia furaha kwa ujio wenu na karibuni sana wakati wowote, Wizara yangu pamoja na nchi yangu kwa ujumla tutaendelea kushirikiana nanyi katika masuala mbalimbali,” Simbachawene.