Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani na mfalme wa Saudia wazungumzia kitisho cha Iran




Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amewatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Saudi Arabia baada ya mazungumzo na Mfalme Salman katika siku yake ya pili ya ziara inayolenga kukabiliana na Iran.

Marekani, ilianza kujenga uwepo wa jeshi lake katika kituo cha anga cha Prince Sultan, kusini mwa Riyadh, mwaka jana kufuatia msururu wa mashambulizi katika eneo la Ghuba ambalo Marekani na Saudia zilisema yalifanywa na adui wao Iran.

Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani imesema ziara ya Pompeo inaonyesha uhusiano wa muda mrefu wa usalama kati ya Marekani na Saudia na unasisitiza dhamira ya Marekani ya kusimama na Saudi Arabia katika wakati ambapo kuna uchokozi wa Iran.

Pompeo alitarajiwa kukutana na Mwanamfalme Mohammed bin Salman na naibu waziri wa ulinzi Mwanamfalme Khalid bin Salman.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad