Wikiendi ya moto kwenye soka, Corona yatia dosari


Wikiendi hii ni ya aina yake kwenye soka duniani ambapo mechi kadhaa kubwa zinatarajiwa kupigwa, lakini dosari kubwa kwa mashabiki kufurahia burudani hiyo inaletwa na tishio la vizuri vya Corona.


Barani Ulaya mechi kubwa katika Ligi Kuu ya Hispania La Liga ni kati ya vigogo wawili Real Madrid watakaokuwa wenyeji wa Barcelona.

Mchezo huo utakaopigwa Jumapili Saa 5:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, mpaka sasa haujawekwa wazi kama kutakuwa na tahadhari yoyote kwa mashabiki juu ya virusi vya Corona.

Barcelona wanaongoza ligi wakiwa na pointi 55, Real Madrid wakiwa na pointi 53 katika nafasi ya pili.

Kwa upande wa Ligi kuu ya Italia mechi kali inatarajiwa kuwa kati ya vinara Juventus wenye pointi 60 dhidi ya Inter Milan waliopo nafasi ya 3 wakiwa na pointi 54.

Hata hivyo mashabiki hawataingia uwanjani kutoka na tishio la virusi vya Corona
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad