Yanga Yanena Kuhusu Mabadiliko ya Mfumo


Uongozi wa klabu ya Yanga umezungumzia hatua iliyopo hivi sasa kuelekea mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaoendelea.


Hayo yanajiri ikiwa ni wiki kadhaa tangu nguli wa mfumo wa soka la kisasa kutoka nchini Ureni, Antonio Domingos Pinto alipokuja nchini kwa ajili ya kuanza mipango ya mabadiliko ya mfumo wa klabu hiyo.

Akizungumzia juu ya mazungumzo yaliyofanyika baina ya uongozi wa Yanga na gwiji huyo, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela amesema kila kitu kinakwenda sawa na wameshafikia muafaka juu ya suala hilo.

“Yeye alikuja kwa mazungumzo ya awali ikiwemo kuiona Yanga ambayo inahitaji kufanya naye kazi na sisi kumfahamu. Sasa kinachoendelea ni kuendeleza pale tulipoishia naye ila kila kitu kimekwenda vizuri,” amesema Mwakalebela.

Ikumbukwe Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dkt. Mshindo Msolla aliahidi mwishoni mwa mwaka uliopita kuwa klabu hiyo itakamilisha mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ifikapo Juni 2020.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad