Zitto Kabwe Ahofia Kukamatwa, Kufunguliwa Mashtaka na Kufungwa Pindi Atakaporejea Nchini


Hofu hiyo inatokana na kile alichokiita mfululizo wa vitisho vilivyotolewa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hofu hiyo ya Zitto imeibuka baada ya Kiongozi Mkuu huyo ACT Wazalendo kuandika barua kwa Benki ya Dunia (WB) kuitaka kusitisha mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa Tanzania kutokana na kile alichodai kuna ubaguzi katika elimu kwa watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Zitto alieleza hofu yake hiyo jana, akidai kuwa analichukulia kwa uzito suala hilo kwa kuwa upo mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kupigwa risasi mjini Dodoma na hadi sasa ameshindwa kurejea nchini kutokana na hofu ya usalama wake.

“Ninachukulia vitisho hivi kwa uzito kwa sababu tuna mfano wa mwenzetu Lissu, lakini usije kushangaa ukisikia nimekamatwa na kufungwa nitakaporejea Tanzania kwa sababu sasa hivi kesi za utakatishaji fedha zinatumika kuwanyamazisha wakosoaji kwa sababu mashtaka yake hayana dhamana," alisema.

Wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, kuchunguza kitendo cha Zitto kuiandikia barua WB kuzuia mkopo huo ili kuona kama kuna jinai au la na kumchukulia hatua mbunge huyo kufuatia hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Siha, DK. Godwin Mollel (CCM), kutaka kuchunguzwa kwa jambo hilo.

Zitto kwa sasa yuko Amerika ya Kaskazini kwa shughuli ambazo chama chake hakijaziweka wazi kwa umma.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jitto Zumbi Kambwe,Hii yoteeni homa na mwewesuko wa uchaguzi wa2020 uukijua Ubunge huupati wanaKigoma na wana Uvira
    wakutolea nje. Na ukimbizi na mazingira unayo yajenga hayana mashiko. Labda wakubebe hawa immigration Lawyers.

    ReplyDelete
  2. Jitto Zumbli Kambwe,Hii yote,ni Homa na muweweseko wa uchaguzi 2020 ukijua fika, Ubunge huupati tena wanaKigoma na wana Uvira wamesha kutolea nje. Na ukimbizi na mazingira unayo yajenga, hayana mashiko. Labda wakubebe hawa immigration Lawyers. Kama Hasiu wako wa miaka ile ya Nyuma CDM. Hivyo yukko wapi??

    ReplyDelete
  3. Jitto Zumbli Kambwe,Hii yote,ni Homa na muweweseko wa uchaguzi 2020 ukijua fika, Ubunge huupati tena wanaKigoma na wana Uvira wamesha kutolea nje. Na ukimbizi na mazingira unayo yajenga, hayana mashiko. Labda wakubebe hawa immigration Lawyers. Kama Hasimu wako wa miaka ile ya Nyuma CDM. Hivyo yuko wapi??

    ReplyDelete
  4. Mie, naona Dogo election fever imempanda upstairs.

    Utaombaje Ukumbizi nchi Nne..??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad