Zitto Asema Uhuru wa Erick Kabendera Umenunuliwa kwa Kukiri Makosa, Watafanya Uchunguzi Huru wa kitaifa



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema amefurahi kwa rafiki yake Erick Kabendera kuwa huru japo uhuru wake umenunuliwa kwa kukiri makosa.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter leo.

Amesema ahadi yake kwa Erick ni kuwa wataifuta hiyo rekodi ya jinai kupitia uchunguzi huru wa kitaifa kwa watu wote walioonewa na kuporwa fedha kupitia mashtaka bandia.

Zitto aliandika ujumbe huu “Nimefurahi sana rafiki yangu @kabsjourno yupo huru. Imebidi Uhuru wa Erick ununuliwe kupitia kinachoitwa kukiri makosa. Ahadi yangu kwa Erick ni kuwa tutafuta hii rekodi ya jinai kupitia uchunguzi huru wa kitaifa kwa watu wote walioonewa na kuporwa fedha kupitia madhtaka bandia,” .

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad