MIJADALA imekuwa mingi sana mtandaoni juu ya kile ambacho kinaendelea katika muziki wa Alikiba, ambaye inaonekana ameshindwa kubadilika na kutoa kazi mfululizo kama ilivyo kwa wasanii wengine.
Mwaka 2020, umeanza kwa kishindo kwa baadhi ya wasanii, ambao tayari wameachia kazi kadhaa ambazo zimekuwa zikifanya vizuri sokoni.
Wasanii kama Harmonize, Rayvanny wameendelea kujiimarisha kwa kufanya kazi nyingi tangu kuanza kwa mwaka huu na wameendelea kuonyesha ushindani ambao unaweza ukaleta matokeo chanya kwa wote wawili.
Mwaka ulianza kwa spidi ya chini sana kwa wasanii kuachia kazi mpya, nafikiri ni kwa sababu wale mafahari wawili katika muziki wa Bongo Fleva, walikuwa hawajaachia kazi yoyote, namaanisha Alikiba na Diamond.
Hatukuona maneno wala posti za kumsifia mtu mmoja huku mwingine akiwa anadharauliwa au kutukanwa kabisa na timu ya upande fulani.
Lakini ghafla, wakati tunakaribia kuumaliza mwezi Februari, likaibuka jambo, hiyo ni baada ya Diamond, kuachia kazi yake mpya, Jeje, iliyotoka Februari 25.
Pengine Jeje, haikuwashtua sana, lakini kilichokuja kuharibu hali ya hewa, ni kusambaa kwa picha na clip za video, Diamond, Babu Tale wakiwa na producer na msanii mkubwa wa Marekani, Swizz Beatz, pamoja na mkewe Alicia Keys ambaye naye ni msanii mkubwa nchini Marekani.
Muonekano ambao ulionyesha dhahiri kuwa kuna jambo linapikwa katika studio za Swizz ambazo ni moja ya studio zinazopika magoma yanayoimbwa duniani kote. Video hizo ziliwaibua watu na mashabiki wa muziki na kuhoji Alikiba anakwama wapi, licha ya wengi kuona ni msanii mwenye kipaji kuliko Diamond!
Kwani kwa sasa imekuwa kawaida kwa Diamond, kumuona akijichanganya nchi tofauti akifanya shoo na kufanya kolabo na wasanii wakubwa.
Unapoitaja Bongo Fleva kwa sasa, lazima umguse na Alikiba, lakini ajabu ni kwamba tangu mwaka umeanza, jamaa yupo kimya kabisa, hakuna ngoma, shoo wala mishemishe ambazo zinaonyesha pengine kuna jambo linakuja kwa upande wake.
Hiyo imekuwa kama msumari wa moto kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakiumia kuona jamaa hana nyimbo mtaani, huku mpinzani wake akiwa anaachia magoma makali kila kukicha.
Kiba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Rockstar Afrika na lebo yake ya Kings Music, yenye memba kama AbduKiba, Ki2ga, Killy na Cheedy, mara ya mwisho kutoa wimbo ilikuwa ni Novemba 8, alipoiachia Mshumaa.
Baada ya hapo akaja na kitu kilichoitwa Unforgettable Tour, hali iliyowapa maneno Team Kiba kuwa kwa sasa msanii wao ameamua kufanya kazi kweli.
Lakini mwisho wa siku ikawa tofauti kabisa kwani tour yenyewe ilifanyika katika mikoa miwili tu, Tabora na Iringa, kisha ikasimama na mpaka sasa hakuna taarifa za nini kinafuatia.
Maswali yamekuwa mengi sana, nini tatizo kwa upande wake, uvivu wa kufanya kazi, majukumu ya kifamilia, biashara au pengine hana menejimenti sahihi, ambayo inaweza kumsimamia kufanya kazi kwa bidii na kwa wakati.
AUNT EZEKIEL AMLIPUA MTANDAONI
Picha aliyoipiga Diamond na Swizz Beats ilimuibua muigizaji Aunt Ezekiel ambaye aliandika maneno kwenye ukurasa wake wa Instagram juzi Jumamosi akidai kuwa jamaa ni mvivu na asiyependa kujituma.
Hiyo ilikuja mara baada ya mashabiki wanaodhaniwa kuwa ni wa Kiba kumshambulia Mondi kuwa ni mshamba na anapenda kujipendekeza kwa wasanii wakubwa.
“Alikiba ndiyo hajawahi kupiga picha na msanii yeyote Marekani, tatizo nyota au uvivu? Mimi nadhani uvivu tu, Alikiba hapendi kujituma hata Konde Boy anamzidi,” aliandika Aunt Ezekiel.Mara baada ya maneno hayo, baadhi ya mashabiki walimjibu kuwa, Kiba siyo mvivu, siyo mshamba kama kupiga picha na mastaa aliwahi kupiga na R. Kelly huku wengine wakidai kuwa, Kiba ndiyo msanii pekee Tanzania asiyekuwa na kiki za kijinga na mambo yake yanaenda.
KUHUSU MENEJIMENTI
Kwa sasa Kiba yupo katika menejimenti mpya, akiwa anasimamiwa kazi zake za muziki na mwanadada Esi Mgimba ambaye amechukua nafasi ya Seven Mosha, ambaye kwa sasa anasimamia baadhi ya biashara za Alikiba na wasanii wengine wa Rockstar Afrika kama vile Ommy Dimpoz.
2020, tayari Ommy ameshafungua na ngoma kali, Kata akiwa na Nandy ambayo ilitoka Januari 3, ikiwa moja ya ngoma zilizosumbua sana YouTube kwa chati za Afrika Mashariki na Kati.
Wakati Ommy akitoa nyimbo nne, Kiba ambaye alikuwa chini ya meneja hiyohiyo, kwa mwaka 2019, alitoa ngoma mbili tu, Mbio iliyotoka April 26 na Mshumaa iliyotoka Novemba 8.
Huenda kwa mwaka jana alisikika kidogo kwa kuwa alikuwa na kolabo na vijana wake wa Kings Music, ngoma kama Kamwambie Sina na Toto, Masozy, na nyingine ilikuwa ni kama sehemu ya kuwatangaza na kuitangaza lebo yake mpya.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Sasa sijui kwa utafiti huo mdogo hapo juu, Alikiba atakuwa anakwamishwa na nini kutoa nyimbo mfululizo kama wasanii wenzake, tatizo ni yeye mvivu kama anavyosema Aunt Ezekiel au menejimenti yake inamuangusha na haijui fitina za soko la sasa la muziki? Tutamtafuta tupige naye stori…