Mbunge wa Hai (Chadema), Freeman Mbowe amewashukia mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo (OCD), akiwatuhumu kuwabambikia raia wema kesi.
Kauli hiyo imekuja miezi michache baada ya Sabaya kuwatuhumu wafanyabiashara wawili mashuhuri kwa kuhujumu miundombinu ya reli lakini polisi mkoani Kilimanjaro wakawasafisha na tuhuma hizo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja ya Snow View, Mbowe ameenda mbali na kumtaka Sabaya na OCD kuacha kuwabughudhi madereva wa bodaboda wanaomuunga mkono.
“DC Sabaya anabambikizia watu kesi zisizokuwa na msingi, anawatuhumu watu kuharibu miundo mbinu ya reli kitu ambacho sio cha kweli, vijana wa bodaboda Hai hawaishi kwa amani eti kisa wanamuunga mkono Mbowe anawaambia eti mtakiona,”
“Eti mnaenda kwenye vituo vya bodaboda kuwazuia wasimpokee mbunge wao mambo gani ya kihuni haya? isitoshe kila mtu anayekuja kwenye mkutano wa Mbowe anasumbuliwa, DC nakwambia utamjua Mbowe ni nani.”
“DC Sabaya usione tunakuogopa, tulikaa mbali tunakucheka tuu, lakini ninamwambie Rais Magufuli ametuletea DC muhuni na kama hutamwondoa sisi watu wa Hai tutapambana naye kihuni,” anasema Mbowe.
Mbunge huyo amedai kuwa wapo vijana wanaojiita ni Sabaya wanatokea Arusha, wamekwenda Hai kunyanyasa wananchi na kuwatesa.
“Tulikaa mbali tukaona utazoea, sasa hutaki kuzoea tutapamba na wewe kwenye majukwaa, sijawahi kuona DC wa sampuli hii. Anaongoza genge la wahuni na siogopi kusema, hao vijana wake wanaojidai ni usalama wa Taifa tunawajua, tunakupa muda jirekebishe , hapa Hai utaondoka kama walivyoondoka Ma- DC wengine,” amesema Mbowe
Amemtaka Ole Sabaya kama anataka kufanya kazi yake vizuri Hai, ni vema akajishusha kwa kuwaheshimu wananchi anaowaongoza na watumishi wenzake wa Serikali.
“Usione madaraka ya kupewa ukaona ni bora kuliko wengine, umechafua na kuidhalilisha wilaya ya Hai na watu wanaogopa kusema, mimi sikuogopi, tunataka Taifa la watu wenye amani na uhuru,” amesema.HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta Mkuu huyo wa Wilaya kusudi azungumzie tuhuma hizo, alisema hawezi kumjibu Mbowe.
Mtowe, mbona unaanza kukosa Adabu.
ReplyDeletestatus yako ktk jamii ni mheshimiwa. jiheshimu usiropoke ropoke kwa homa ya uchaguzi. Sabaya Baba Lao.