Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amempongeza msanii wa muziki wa Hip Hop Mwana FA kwa kumuona yeye kama ni jasiri na kwamba ataweza kupambana na kuushinda ugonjwa wa Corona.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Waziri Ummy, alimpa pole Mwana FA masaa machache tu tangu aamue kuiweka wazi hali yake ya kiafya kwa sasa, mara baada ya hapo jana Machi 19, 2020, kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.
"Ugua pole mdogo wangu MwanaFA, hakika wewe ni kijana jasiri, sina shaka kuwa utaishinda Corona #PamojaTunavukaSalama ##covid19Tanzania" ameandika Waziri Ummy.
Mwana FA aliwatoa hofu Watanzania na kuwataka wazingatie kanuni bora za afya kama zinavyoelekezwa na wataalam.