Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Tanzania (LATRA) imeyataka mabasi ya usafirishaji abiria maarufu 'daladala' katika mikoa yote Nchini kubeba watu kulingana na idadi ya siti zilizopo
Imetoa maagizo hayo baada ya kukutana na wadau wa usafiri na usafirishaji, kutafakari na kuweka mikakati ya kukabiliana na kasi ya kusambaa kwa #COVID19
Pia, magari hayo yanapaswa kunyunyiziwa dawa kila mwisho wa safari na kuwa na dawa ya kuua wadudu mikononi (hand sanitizer) ili kila abiria apake kabla ya kuingia
Mabasi yaendayo haraka (BRT) yametakiwa kubeba idadi ya abiria kulingana na idadi iliyoainishwa kwenye leseni zao na magari ya mizigo hayaruhusiwi kubeba abiria
Shirika la Reli Tanzania (TRC) wametakiwa kuhakikisha treni zinapuliziwa dawa za kuua virusi kila mwisho wa safari na abiria wanapoingia Kituoni kunawa kwa sabuni na maji tiririka
Aidha, Waendesha taksi, pikipiki za magurudumu mawili na matatu wametakiwa kuhakikisha abiria wanapaka dawa ya kuua virusi mikononi (hand sanitizer) kabla ya kupanda kwenye chombo husika