ACT-Wazalendo wataka uchambuzi virusi vya corona ufanyike


 Chama cha ACT- Wazalendo kimeitaka Serikali ya Tanzania kufanya uchambuzi juu ya madhara ya mlipuko wa virusi vya Corona katika uchumi wa nchi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na matokeo hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hichokiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe amewaomba wajumbe kuazimia kutoa maagizo hayo kwa Serikali.

Amesema Serikali haina budi kuchukua tahadhari kwani kulingana na hali ya huduma zetu za kiafya endapo ugonjwa huo utatua nchini utakuwa na athari kubwa kwa Taifa.

“Hakuna Mtanzania ambaye ameripotiwa kuathiriwa na ugonjwa huo lakini virusi vyake vimesambaa nchi nyingi duniani na kuna maelfu ya Watanzania wanakaa China, tuwaombee kwa Mungu ili waendelee kuwa salama,” amesema.

Vilevile, Zitto amesema China ni mshirika mkubwa wa uchumi wa Tanzania katika biashara na uwekezaji na virusi vya Corona vitakuwa na athari katika uchumi hivyo Serikali inapaswa kufanya uchambuzi na kuwaeleza wananchi namna ambavyo itakabiliana na changamoto hizo.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nani anaempa Airtime, huyu mzamiaji na msaliti asie itakia mema nchi yetu.
    Naona kichefu chefu mwana twita mwacheni huko huko tukimtaka tutapiga hodi kote tiki toki, fwezibuku n twita.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ati nasikia kumenuka na upande ule ..baada kumrubuni mtundu antipasi na kumsha wishi ajiuge na maalim. Hivyo kweli yamejiri haya!!

      Delete
  2. Nani anaempa Airtime, huyu mzamiaji na msaliti asie itakia mema nchi yetu.
    Naona kichefu chefu mwana twita mwacheni huko huko tukimtaka tutapiga hodi kote tiki toki, fwezibuku n twita.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tena wakiweka hii sura ya buriani ndiyo kabisaaaaa.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad