Afisa wa magereza amuua kinyama mpenziwe waliyepatana kwenye Facebook


Polisi katika Kaunti ya Kiambu wamemkamata mwanamume mmoja ambaye anatuhumiwa kwa kumuua mpenzi wake mnamo Jumatano, Februari 26, katika eneo la Ruaka.

Tairus Mwangi, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ni afisa wa magereza katika Gereza la Malindi, Kaunti ya Kilifi , anakisiwa kumpiga Purity Karwirwa mara kadhaa kwenye kichwa, pua na mgongo akitumia nyundo.

Mwangi na marehemu Karwirwa ambaye aliyekuwa na miaka 26, walichumbiana kwa kipindi cha mwaka mmoja unusu baada ya kukutana kwenye Facebook, huku uhusiano wao ukizingirwa na mgogoro wa kila mara kama alivyofichua nduguye Karwirwa, Erick Kimathi.

Kimathi alifuchua kwamba, dada yake ambaye alikuwa anajipatia kipato kupitia kwa uandisi mtandaoni, alikuwa akimtembelea mpenzi wake mjini Malindi kila mara.

“Uhusiano wao ulikuwa umezingirwa na dhuluma, huku mshukiwa akiwa na hasira kila mara," alikariri Kamithi kama alivyonukuliwa na K24 siku ya Jumamosi, Februari 29.


Kulingana na Ndugu yake Karwirwa, marehemu alikuwa akiishi na swaiba wake katika eneo la Donholm, jijini Nairobi.

Rafiki huyo aliyetambuliwa kama Skitter Ntinyari, alifichua kuwa kila mara Karwirwa alikuwa akigombana na mpenzi wake kila mara wakiwasilina kwenye simu.

Kabla ya tukio, mshukiwa anasemekana kuwasili Nairobi mnamo Jumatano, Februari 25, na kuomba kukatana na Karwirwa ili kutatua tofauti zao ambapo marehemu alikubali na kisha Mwangi alikwenda kumchukua mpenzi wake kutoka kwa swaiba wake eneo la Donholm.

Mshukiwa anadaiwa kumpiga marehemu akitumia nyundo kwa kumgonga kwenye kichwa, pua na mgongo mara kadhaa.
Inadaiwa Mwangi alifululiza na Karwirwa hadi kwa dada yake eneo la Ruaka, siku ya Jumatano, Februari 26 ambapo tena walitofautiana na kumpelekea Mwangi kuchukua nyundo na kumgonga Karwirwa kwenye kichwa, pua na mgongo mara kadha na kisha kumuua papo hapo.

Kamera ya CCTV katika eneo la tukio inamuonyesha Mwangi akiondoka nyumbani kwa dada yake baada ya kubadilisha nguo zake.
Dada yake mshukiwa alishtuka kufika kwake siku ya Jumatano na kupata mwili wa Karwirwa ukiwa umelowa damu na kisha kupiga ripoti katika Kituo cha Polisi cha Karuri na kuanzisha msako wa kumtafuta mshukiwa aliyekuwa ameingia mitini.

Makachero wa DCI waliweza kufuatilia hatua za mshukiwa ambaye aligunduliwa kuwa katika baa moja eneo la Kahawa West siku ya Alhamisi, Februari 27, ambapo alikamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polisi cha Karuri ambapo anazuiliwa.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Matokeo ya upasuaji uliofanyiwa mwili wa Karwirwa mnamo Ijumaa, Februari 28, ulitambua kwamba marehemu alifariki kutokana na majeraha kwenye kichwa.

Mwili wa Karwirwa ulisafirishwa hadi katika kijiji cha Mwaniki, Imenti ya Kati, Kaunti ya Meru kwa mazishi huku mshukiwa akitazamiwa kufikishwa kortini Jumatatu, Machi 2, uchunguzi ukiendelea.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad