Halima Mdee "Mama Yangu Usilie Kesho ni Nzuri Kuliko Jana Nakupenda Sana"



Mbunge wa Kawe kupitia chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA Halima Mdee amemempa ujumbe wa kumtia moyo mama yake mzazi ambaye alikua akionekana akilia mahakamani wakati akisikiliza hukumu yake pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA.

Kupitia akaunt yake ya twitter aliandika hivi;
Mamie wangu kipenzi.... umekuwa MHIMILI Mkubwa kwangu katika harakati HIZI za kupambania DEMOKRASIA...usilie... kesho ni NZURI kuliko JANA!!!!! Nakupenda SANA!!
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Mhe.Grace Tendega akimpa pole mama yake Mwenyekiti wa BawachaTaifa Mhe. Halima Mdee, mda mchache kabla ya kuanza kusikilizwa kwa hukumu ya kesi 112/2018 inayomkabili Halima Mdee pamoja  viongozi wenzake na baadhi ya wabunge wa chama hicho

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad