Mnyika, Heche na Mwalimu Watoka Jela


Dar es Salaam. Viongozi watatu wa Chadema waliokuwa gereza la Segerea wametoka leo Ijumaa  Machi 13, 2020 saa 3:50 asubuhi baada ya kukamilisha kulipa faini.
Viongozi walioachiwa ni Katibu Mkuu, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu na mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mpaka sasa viongozi wote wa Chadema wametolewa jela isipokuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ambaye mpaka sasa bado hatma yake haijajulikana.

Viongozi wengine wa Chadema ambao wameachiwa ni wabunge Halima Mdee (Kawe), Esther Bulaya (Bunda Mjini), Esther Matiko (Tarime Mjini) na Peter Msigwa (Iringa Mjini).
Chama hicho kimechangisha fedha kutoka kwa wanachama wake na watu wengine ambao wameguswa na hukumu ya viongozi hao.

Baadhi ya wanachama waliokuwepo katika gereza la Segerea wakisubiri kuachiwa huru kwa viongozi hao wamesema wamefurahishwa kuachiwa kwa viongozi wao ili waendeleze mapambano ya kisiasa.

"Hivi vitendo vya dhuluma vina mwisho wake, Chadema tumeonyesha mshikamano mpaka dakika ya mwisho. Na hii ndiyo nguvu ya umma," amesema kada wa Chadema, Abubakary Kaisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad