Alichokisema Mama Rwakatare Kuhusu Ugonjwa wa Corona


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Askofu Getrude Rwakatare, amesema kuwa ametenga siku tatu kwa ajili ya maombi ya kuzuia ugonjwa wa homa kali unaosababishwa na Virusi vya Corona, usiingie nchini na hata pia usiendelee kuenea kwenye Mataifa mengine.


Mchungaji Mama Rwakatare ameyabainisha hayo wakati wa Ibada ya Jumapili, Kanisani kwake Mikocheni B na kusema kuwa ibada hiyo ya kufunga na kuomba itaanza leo Machi 16 hadi 18, 2020.

"Kama kweli sisi tu watu wa Mungu, lazima tutii sauti ya Rais wetu na ndio maana tunatangaza siku tatu za kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa letu, mnakumbuka tuliomba kwa ajili ya Nzige wasiingie Tanzania, Mungu akatujibu, kama Nzige hawakuingia Tanzania, inawezekana pia tukiomba Corona isiingie Tanzania" amesema Mchungaji Mama Rwakatare.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad