Doreen Odemba ni binti ambaye aliamua kuiweka wazi hali yake ya kiafya ya kuwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI , ameeleza ni kwa namna gani mpenzi wake alivyotaka kumgeuza kuwa kitega uchumi, hali iliyopelekea wao kuachana.
Akizungumza kwenye kipindi cha DADAZ kinachorushwa kila siku ya Jumatatu hadi ijumaa, saa 5:00 Asubuhi hadi saa 6:00 Mchana, Doreen amesema kuwa licha ya kwamba uwazi wake umewasaidia watu wenye maambukizi hayo, ikiwa ni pamoja na wao kujikubali hali zao.
''Nilikuwa kwenye mahusiano lakini hayakuwa sahihi, maana alipoona harakati zangu hizi akaona ni nafasi ya yeye kutoka kimaisha akawa ananililia shida kila siku, mara hana hiki mara kile kwahiyo tukaachana'' - Doreen Odemba.
Doreen Odemba alizaliwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, na aliamua kujitangaza kwa lengo la kudhibiti unyanyapaa kwa watu hao na kwamba kuwa na ugonjwa huo siyo mwisho wa maisha.