Arusha: Kilichojiri kwa dereva tax aliyembeba mgonjwa wa Virusi vya Corona, Isabella



Dereva wa tax aliyembeba mgonjwa wa kwanza wa Virusi vya Corona mkoani Arusha, sampuli ya vipimo vyake kutoka maabara, zimeonesha kuwa hana maambukizi ya virusi hivyo.


Msemaji wa Wizara ya Afya wa masuala ya Corona Mkoa wa Arusha, Dkt Janeth Mghamba

Taarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Afya wa mambo yote, yanayohusiana na Ugonjwa wa Corona kwa upande wa Mkoa wa Arusha Dkt Janeth Mghamba na kusema kuwa, Serikali ilichukua juhudi za makusudi kabisa za kuhakikisha zinawapata wale wote waliokutana na dereva huyo na kuwafanyia vipimo.

“Waliokuwa wakifuatiliwa ni 27 pamoja na dereva, sampuli zao zote zilichukuliwa na zote zimeonekana hazina Virusi vya Corona na majibu haya yamechukua muda kwa sababu vipimo hivi vinaangaliwa zaidi ya mara moja na tumejiridhisha kwa kina baada ya kuviangalia mara tatu, bado tutaendelea kuwa nao kwa muda wa siku 14” ameeleza Dkt Janeth.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad