Aslay Awaka Kuzushiwa Kumpiga Mzazi Mwenzie



Msanii wa bongo freva maarufu kama Aslay amesikitishwa na kukanisha tuhuma za kumpiga mzazi mwenzie Sonia na kudai kuwa kuna mpango unapangwa ili kumchafua.

Kupitia akaunti yake ya instagram ameposti sauti nambayo ya mzazi mwenzake akimuhoji kama amempiga huku sauti hiyo ikikana Aslay kufanya tukio hilo.

Baad ya kupost audio hiyo aslay aliandika maneno haya;

Nimesikitishwa sana na vitendo vya kupangwa, vyenye nia mbaya dhidi yangu vinavyoendelea. Inasikitisha zaidi, Media (Online Media) inapojiingiza kwenye michezo michafu ya hovyo kwa faida nisizojua (yaweza kuwa wamepewa pesa au wana sababu zao nyingine). #GlobalOnline wamenikosea sana, sijui mtu anayeheshimika kama #EricShigongo anawezaje kuajiri watu wasio na weledi, wakaenda kushiriki kwenye habari za uzushi namna hii tena za kupangwa. Jioni ya leo wamesambaza video ya kupikwa, ikidai kwamba eti mimi nimempiga Mzazi mwenzangu (Sonia). Ni habari ya kizushi mno, sijamgusa kwa namna yoyote. Ninachokifahamu kuna watu walifika nyumbani kwangu na kuanza kufanya fujo kwa sababu zao, pengine ilikuwa kunilazimisha kufanya vitendo vya ajabu kwa hasira wakimtumia Sonia, na kumshawishi aseme uongo. Nashukuru Mungu sikufanya kitu chochote kibaya.
.
Nilimpigia Sonia kuuliza nini kimetokea, mwenyewe anashangaa japo anakiri wapo watu wanaomshawishi kuongea uongo mwingi kuchafua jina langu.
.
Sitaongea mengi, najua ukweli utajulikana tu. Kinachosikitisha sana kwangu na kwetu kama jamii, ni jinsi vyombo vya habari vinavyoweza kutumika kusambaza uongo, chuki na kuharibu majina ya watu na biashara zao. Walioko nyuma ya michezo hii michafu tunawafahamu, na wao wananifahamu, wakati utawambua, NA MUNGU PEKEE NDIYE SHAHIDI WA KWELI.
.
Asanteni

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad