ATCL yasitisha Safari za Ndege China
0
March 12, 2020
Shirika la Ndege Tanzania ( ATCL) limetangaza kusitisha safari za ndege kuelekea China kutokana na kuwapo kwa ugonjwa wa virusi vya Corona.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mkutano wa tano wa baraza la wafanyakazi la shirika hilo.
Ladislaus Matindi amesema changamoto inayolikabili shirika hilo ni pamoja na baadhi ya viwanja vya ndege kutokuwa na taa, kutokuwa na vyumba vya kuhifadhia mizigo hususani inayohitaji ubaridi, pamoja na ubovu wa miundombinu.
Wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amesema mojawapo ya athari zinazotarajia kutokea nchini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Corona ni pamoja Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kukosa abiria, kupungua kwa bidhaa.
Kwa mujibu wa Nipashe, Mhe. Nditiye amesema Tanzania haina mpango wa kuzuia ndege za mataifa mengine kuingia nchini kutokana kuwapo wa ugonjwa wa virusi vya virusi vya Corona bali itaboresha upimaji wa abiria raia wa kigeni wanaongia.
Tags