Baada ya Kufulia Kwa Muda Mrefu , MR Nice Amerejea na Cheche za Maneno Kuntu


Kwa wakati mmoja alidhaniwa kuwa mwanamziki ambaye angetetemesha mawimbi ya sanaa ya muziki kutoka Tanzania ,lakini baada ya kutoo nyimbo kama Kikulacho na Fagilia ,Mr Nice alisemekana kuishiwa na pesa kwa kile waliseme kuwa alikuwa anaishi maisha ya kifahari yaliyomfanya kufilisika na hata wakati mmoja kufungiwa nyumba.

Kwa muda sasa,paparazzi walikuwa wanasema kuwa Mr Nice alikuwa anaishi maisha ya kuomba misaada kutoka kwa wasanii wenzake ili kujikimu kimaisha.

Hivi maajuzi akizungumza na mwanahabari mmoja wa mitandao wa Tanzania ,Mr Nice amekiri kuwa yuko na mihela ya kutosha inayomfanya kuendelea kuishi maisha ya kifahari na hata kujiburutisha katika mikahawa na baa maarufu Tanzania.

Nam niko na pesa sasa na ndio maana naishi maisha ya kifahari ,ukitaka kuishi na maisha ya raha mustarehe lazima uwe na donge nono la hela.Lazima utermbee na pesa kwa sababu utafika maeneo fulani ambayo hayana benki za kusitiri pesa zako ,utaweka wapi kwa gari ama kwa buti?.alismulia Mr Nice

Mr Nice katika mazungumzo hayo aliongeza kuwa.

Nimefanya kile watu wengi wamefanya kama kuwa na magari ,kuvalia nguo za kifahari ,natembea na pesa kwenye buti la magari langu ,wewe unaweka hela zako kwenye kibeti na unadai uko pesa,aliongezea Mr Nice

Wakati mmoja akiwa na mazungumzo na televisheni moja ,Mr Nice alikiri kuwa hana pesa za kukithi maisha yake na familia ,na hata wakati mmoja akawataka wafuasi wake kumsaidia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad