Bibi wa miaka 70 adaiwa kubakwa hadi kufa


Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Mwanamke mmoja Mkazi wa Area A Mtaa wa Sokonne Jijini Dodoma anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 (Jina limehifadhiwa) amefariki dunia baada ya kudaiwa kubakwa hadi kufa na watu wasiojulikana wakati akielekea kanisani majira ya alfajiri.

Akizungumza kwa njia ya simu kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kikongwe huyo alifanyiwa kitendo hicho majira ya saa 11:45 asubuhi wakati akielekea Kanisa Katoliki la Bikira Maria msaada wa Kristo lililopo mtaa wa Area A.

Amesema jeshi la Polisi lilipata taarifa za kifo hicho majira ya asubuhi leo na Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kuwasaka watu waliomfanyia kitendo hicho kikongwe huyo.

 "Tunashukuru wananchi kwa kutoa ushirikiano hivyo jeshi la Polisi linaendelea kusaka wahalifu waliotenda kosa hilo, " amesema Muroto.

 Mwenyekiti wa mtaa wa Soko nne eneo la Area A, Joshua Temu amesema alipokea taarifa majira ya saa 12 alfajili  kuwa kuna mtu amelala kwenye majani kwenye eneo la wazi.


“Baada ya kupokea simu hiyo nilitoka nikaenda eneo alilolala mtu huyo na kukuta tayari amefariki huku akiwa amevuliwa nguo za ndani zikiwa pembeni na biblia yake ikiwa pembeni,”amesema bw. Temu.

 Ameliomba jeshi la polisi kufanya msako mkali kwenye eneo hilo ili kukomesha vitendo vya uhalifu ambavyo vimekithiri kwa siku za hivi karibuni katika mtaa huo.

“Inasikitisha kuona vijana wanawaua wazee wa rika hili kwa kuwabaka badala ya kuacha waishi mpaka muda utakapowadia, tumechoshwa kusikia vitendo hivi,”amesema.

Kwa upande wake Jirani wa marehemu, Innocent Lugusi amesema wamesikitishwa sana na tukio hilo na kuliomba Jeshi la Polisi kufanya utaratibu wa doria katika eneo hilo.

"Kumekuwa na matukio tofauti ya kiuhalifu hapa Area A tunaomba jeshi la Polisi kusaidiana na wananchi kuwasaka wahalifu," amesema Lugusi.

Hata hivyo, amesema wao kama raia wa mtaa huo wanajipanga kuanzisha ulinzi shirikishi kwa ajili ya kujilinda katika eneo hilo kuepukana na vitendo hivyo.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ulinzi Shirikishi ni Jibu sahihi..
    pia Wahuni nna wauza majani ya bange Changombe ni changamoto ambayo Kamanda
    Muroto asiifumbie macho ni lazima aje na utatuzi maana ni Adhaa kubwa inayo
    tukabili wakazi wa haya maeneo licha ya kuwa na polisi post tupu.

    Si aibu kujifunza Mrema alikomeshaje vitenndo hivi na Tanzania yetu ilikuwa Saama zaidi mijini na Vijijini.

    Poleni Wafiwa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad