Bodaboda, Daladala Marufuku Uganda, VITA Dhidi ya Virusi vya Corona
0
March 26, 2020
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amepiga marufuku matumizi ya usafiri wa umma nchini Uganda.
Katika hotuba yake kwa taifa, bwana Museveni alitangaza marufuku katika usafiri wote wa umma ikiwemo boda boda.
Mabasi madogo na yale makubwa yanayoelekea maeneo ya mashambani pamoja na magari moshi pia yamepigwa marufuku.
Magari ya kibinafsi yanaweza kutumika lakini sasa yatalazimika kubeba watu watatu pekee akiwemo dereva.
Masoko nayo yatasalia wazi lakini yatakuwa yakiuza vyakula peke yake.
Hatua hiyo inajiri baada ya taifa hilo kuthibitisha visa vingine vitano vya ugonjwa wa coronavirus kikiwemo kisa cha mtoto mwenye umri wa miezi minane na hivyobasi kufanya visa hivyo katika taifa hilo kufikia idadi ya watu 14.
Wiki mbili zilizopita serikali ya Uganda ilizindua sera ya karantini ya lazima kwa wasafiri wanaowasili nchini humo kutoka mataifa 16 yaliyopo katika ‘hatari zaidi’ ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Corona.
Uingereza, Marekani na nchi kadhaa za Ulaya ni miongoni mwa mataifa yatakayoathiriwa na sera hiyo mpya ya usafiri nchini Uganda.
Wiki iliyopita taifa hilo la Afrika Mashariki lilitangaza hatua kama hiyo dhidi ya mataifa saba.
Serikali pia ilisema kwamba wasafiri wanaowasili katika uwanja wa kimataifa wa Entebbe hivi karibuni watakuwa wakipuliziwa dawa.Boda boda nchini Uganda
Hatua ya kudhibiti wageni wanaowasili nchini Uganda kutoka mataifa yanayokabiliwa na ugonjwa huo inamaaninisha Covid-19 haitawaathiri watu wengi ikiwa mtu yeyote aliyeambukizwa atashughulikiwa ipasavyo.
Kwanini Uganda iliwafurusha raia 22 wa kigeni waliowasili kwa kongamano la kibiashara
Maafisa wa wizara ya afya nchini Uganda mnamo tarehe tisa mwezi Machi walisema kwamba takriban raia 22 wa kigeni waliriudishwa katika mataifa yao huku hofu ya maambukizi ya virusi vya corona ikiendelea.
Uganda ndio iliokuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa kuhusu biashara lililoanza nchini humo wiki tatu zilizopita
Kwa mujibu wa waziri ya afya nchini humo raia hao walikataa kwenda karantini kwa siku 14 walipowasili katika uwanja wa ndege wa Entebbe.
Aidha hakuna hata mmoja wao aliyekuwa na dalili ama ishara za COVID19. “Tuliwaambia kuhusu hatua zetu za kujiweka katika karantini kwa siku 14 .
Hatahivyo hawakuwa tayari kufuata maagizo yetu .Hii leo watarudi nyumbani kwao”, waziri wa afya Dkt. Ruth Aceng alisema sikjuya Jumapili. ”
Hatua hiyo ya Uganda ilijiri saa chache tu baada ya mtalii kutoka Ujerumani kufariki kutokana na virusi vya corona katika eneo la kitalii la Sinai mashariki mwa Misri, ikiwa ndio kifo cha kwanza kurekodiwa Afrika.
Raia huyo wa Ujerumani aliyekuwa na mwenye umri wa miaka 60 alionyesha dalili za joto mwilini na kulazwa katika hospitali ya Hurghada tarehe 6 mwezi Machi , kabla ya kupatikana na ugonjwa huo , ilisema ripoti ya wizara ya afya.
Mtalii huyo aliyewasili kutoka Ujerumani wiki moja iliopita , alifariki baada ya kukataa kuhamishwa hadi katika eneo lililotengwa baada ya kuugua ugonjwa mbaya wa mapafu.
Siku ya Jumamosi , wizara ya afya ilitangaza kuhusu visa 45 vya raia wa Misri na wale wa mataifa ya kigeni waliodaiwa kuambukizwa virusi hivyo katika meli moja mto Nile
Tags