Boss Aliyemuua Mfanyakazi wa ndani Kufikishwa Mahakamani leo



Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kuwa baada ya kumhoji kwa kina mtuhumiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa ndani, aliyejulikana kwa jina la Salome Zacharia, amekiri kufanya kitendo hicho na atafikishwa mahakamani siku ya kesho (leo).

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Jonathan Shanna, na kusema mtuhumiwa huyo aliyejulikana kwa jina la Mkami Shirima, alimpiga binti huyo na kisha kumfungia ndani kwa siku mbili, ambapo baadaye alizidiwa na kumkimbiza hospitali na ndipo mauti yalikomkuta.

"Marehemu alifariki Dunia Machi 9, katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake, tumemhoji mtuhumiwa kwa kina na amekiri, upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kesho Machi 13, 2020, atafikishwa mahakamani" amesema ACP Shanna.

Aidha ACP Shanna amesema kuwa mwili wa marehemu umesafirishwa leo, kwenda mkoani Singida kwa ajili ya mazishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad