Breaking News: Mwana FA Akutwa na Virusi vya Corona



RAPA maarufu wa Bongo, Hamisi Mwijuma, maarufu Mwana FA amethibitisha kuwa amepimwa na kukutwa ameathirika na virusi vya COVID- 19 au Corona.


FA amesema alifanya vipimo hapo jana na kupatiwa majibu yake hii leo vilivyobainisha kuwa ameathirika na virusi hivyo. Katika kipande chake cha video alichokiweka kwenye mitandao ya kijamii, Mwana FA amesema alitoka Afrika Kusini juzi na kubaini kuwa joto lake la mwili halikuwa la kawaida.


”Sababu ya kufanya hivyo nilikuwa natoka safarini Afrika Kusini, joto langu la mwili lilikuwa halieleweki, linapanda, linashuka hivyo nilivyorudi kwa sababu habari duniani inayofahamika ni hiyo nikawa nimejitenga ili kuhakikisha siwaathiri watu wengine.
“Majibu ya vipimo vyangu vya Covid 19 yamerudi chanya. Inaudhi. Siumwi KABISA. Nipo sawa 100%. Na nimejitenga toka niliporudi ili kuepuka kuathiri wengine. Na kwa bahati hata watoto wangu sijakutana nao kabisa. Hawapo nyumbani.
“Nawaomba tu tuchukue tahadhari kwa kadri ya uwezo wetu kukwepa usitupate na hata tukipatwa nao sio tatizo la kivile kwani virusi wake wanaondoka wenyewe baada ya siku kadhaa tu. So yah, sisi wa nchi hizi tulioandamwa na migonjwa mikubwa-mikubwa katika kukua kwetu, haya ‘mafua’ wala si kitu cha kututisha. ITAKUWA TU SAWA. Tuweni na amani tu mioyoni,” amesema FA.
Mwanamuziki huyo amesema kwa sasa ile homa aliyokuwa akiihisi juzi kwa sasa haipo tena lakini bado amejitenga wakati afya yake ikiendelea kuimarika. Hapo awali meneja wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam SK , naye alithibitisha kuwa amekutwa na virusi vya Corona na sasa yupo chini ya uangalizi na afya yake inaendelea vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad