China : Watanzania Wanaoishi Huku Wapo Salama



Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke amewahakikishia Watanzania kuwa ndugu zao waishio nchini humo wako salama.

Amefafanua kuwa wanafunzi wanaosoma katika vyuo vilivyoko Wuhan wako katika uangalizi kuhakikisha vyuo hivyo vimeendelea kuchukua tahadhari kubwa kuwakinga wasipate maambukizi ya virusi vya Corona.

Ugonjwa huo unaosababishwa na virus vya Covid - 19 tayari imesababisha vifo 2946.

Balozi Wang Ke ametoa kauli hiyo mjini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa kamili kuhusiana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa umesababisha maambukizi kwa wagonjwa 80,000 huku bara la Afrika likitajwa kuwa na wagonjwa 9.

Amewatoa hofu watanzania na kusema kwamba ubalozi wa Tanzania nchini China umekuwa ukifanya mawasiliano ya mara kwa mara na vyuo wanavyosoma watanzania ili kujiridhisha kuhusu ya usalama wao.

Balozi Wang Ke amesema kwa sasa maambukizi ya ugonjwa huu yamekuwa yakipungua na kuonyesha matumaini makubwa, ambapo amasema hali hii imetokana na uongozi madhubuti uliopo nchini humo.

Akizungumzia athari za kiuchumi amekiri taifa hilo kupata mtikisiko kufuatia kusimama kwa shughuli za uzalishaji na kukosekana kwa mwingiliano wa kibiashara.

Lakini ameeleza matumaini yake kuwa mara ugonjwa huo utakapoisha shughuli za kiuchumi zitaendelea kama kawaida.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad