Wahenga walisema ‘Ujana maji ya moto’, usemi huu unaendana na alichosema Mwanamitindo Chrissy Teigan aliyejilaumu kwa kufanyiwa upasuaji wa matiti akiwa na umri wa miaka 20.
Alisema kwa sasa anajikuta yupo katika wakati mgumu kutokana na kupata watoto ambao wanahitaji maziwa ya mama na yeye hawezi kuwanyonyesha.
Akihojiwa na Jarida la Glamour la Uingereza, mama huyo wa watoto watatu alifunguka kuwa anajilaumu kwa maamuzi aliyoyafanya akiwa bado kijana.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa, alisema alifanya hivyo ili atokee vizuri katika picha alizokuwa akipiga akiwa amevaa nguo za kuogelea.
“Nilifanyia upasuaji matiti ili nikipiga picha nimegeuza mgongo kidogo, matiti yaonekane vizuri kwa pembeni ya nguo za kuogelea ambazo huwa wazi sehemu kubwa ya kwapani,” alisema.
Alifafanua anapaswa kuyafanyia marekebisho matiti yake kila baada ya miaka 10, lakini alipopata watoto anafikiria mara mbili kwenda kufanya upasuaji huo.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>
“Sasa hivi ninachukulia suala hilo kama hatari, ninafikiria watoto wangu, familia yangu sihitaji kufia katika chumba cha upasuaji au kupata madhara yatokanayo na suala hilo,”alisema.
Teigan alifanya upasuaji kuyajaza maziwa yake na yawe na mwonekano kama kikombe.