Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona (Covid-19) katika nchi za Afrika Mashariki za Uganda na Rwanda imepaa kwa kasi huku nchi hizo zikipambana kuzuia maambukizi zaidi.
Nchini Uganda jana usiku wametangaza wagonjwa wapya nane na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia tisa.
Wagonjwa hao wapya wanane wote ni raia wa Uganda ambao wamerejea nchini humo kutokea Dubai baina ya tarehe 20 na 22 mwezi huu.
Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng amewaambia wanahabari kuwa kufikia sasa nchi hiyo imebaini wasafiri 2,661 wakiwemo raia wa nchi hiyo ambao wanaweza kuwa na hatari ya kusambaza maambukizi na watu wote hao wapo chini ya uangalizi maaalumu.