Rais wa Marekani Trump anadai dawa inayotumiwa dhidi ya malaria imeithinishwa nchini Marekani kutibu coronavirus mpya.
Chloroquine ni moja ya madawa ya zamani sana yanayofahamika sana kutibu ugonjwa wa malaria.
Kwahivyo je rais ni sahihi na ni kipi kinafahamika juu ufanisi wake wa kimatibabu?
Chloroquine imekuepo kwa miongo kadhaa. Haitolewi tena katika mataifa mengi ya Afrika kwasababu ya kinga iliyojengwa na wadudu wa malaria.
Baadhi ya nchi zimetoa sheria ya kukabiliana na matumizi ya dawa hiyo, lakini imebakia kuwa maarufu miongoni mwa wale wenye sekta binafsi ya soko la madawa na inauzwa kwa kiwango kikubwa.
Hii ni dhahiri hasa nchini Nigeria ambako kumekua na ripoti za chloroquine kununuliwa sana katika maduka ya dawa na hivyo kusababisha upungufu, na kwa sehemu kubwa upungufu huo umechochewa na kauli ya Bwana Trump.
Chloroquine bado haijaidhinishwa kwa tiba ya coronavirus
Rais Trump, katika mkutano wa kila siku na waandishi wa habari, alidai kwamba chloroquine imeidhinishwa kwa kwa ajili ya kutumiwa kwa matibabu ya coronavirus na Taasisi ya Marekani ya masuala ya Chakula na Dawa (FDA). Taasisi hiyo inahusika na utoaji wa vibali vya dawa nchini Marekani.
"Tutaweza kuwezesha upatikanaji wa dawa hiyo mara moja. Na hapo ndio FDA imekua bora. Wamepitia mchakato wa kuiidhinisha - imeidhinishwa."
Kusema wazi, chloroquine imeidhinishwa kutibu magonjwa ya malaria ugonjwa wa viungo (arthritis). Hatahivyo, FDA imeweka wazi dawa hiyo haitibu watu Covid-19 coronavirus.
" Hakuna idhini ya FDA- ya matumizi ya dawa hiyo kutibu au kuzuwia Covid-19."
Hatahivyo, FDA inasema kuwa utafiti unaendelea kuangalia ikiwa chloroquine inaweza kutibu Covid-19. Imesema pia kwamba imeagizwa na Bwana Trump kuanzisha kliniki ya majaribio ya kimatibabu ili kuichunguza dawa hiyo.
Vipi kuhusu hali ya utafidi wa dunia juu ya coronavirus?
Haishangazi kwamba chloroquine imekua ni sehemu ya utafiti wa kuwasaidia wagonjwa wa coronavirus
Inafahamika sana, na ni nafuu na rahisi kutengeneza. Katika kuwatibu wagonjwa wa Malaria, dawa hiyo imekua ikitumika kupunguza joto la mwili na vidonda.
"Chloroquine ilionekana kuzuwia coronavirus katika tafiti za maabara. Kuna ushahidi kiasi kutoka kwa madaktari wakisema kuwa imeonekana kusaidia " anasema James Gallagher, Mwandishi wa BBC wa masuala ya afya.
Lakini la muhimuni kwamba hakuna ushahidi kamili wa majaribio ya tiba ambao umekamilika ambayo ni muhimu kuonyesha jinsi dawa inavyofanya kazi katika mgonjwa halisi, ingawa yanafanyika katika mataifa ya Uchina, Marekani, Uhispani na Uingereza.