Mtu tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote hatimaye amepatiwa bei ya kuinunua klabu ya Ligi kuu ya England Arsenal.
Bilionea huyo wa Nigeria awali alikuwa ameonyesha hamu yake ya kutaka kuinunua klabu hiyo ya kaskzini mwa London.
Dangote anasema kwamba kwa sasa anaangalia maslahi mengine , lakini analenga mwaka ujao kuzindua ombi lake la kuinunua klabu hiyo kulingana na gazeti la Miror Uingereza.
Mwezi Januari , alisisitiza, malengo yake akisema: Ni klabu ambayo kweli ningependa kuinunua siku zijazo, lakini kile ninachosema ni kwamba tuna miradi yenye thamani ya dolla bilioni 20 na hilo ndio ninaloaangazia kwa sasa.
''Ninajaribu kumaliza kujenga kampuni hiyo , halafu baada ya kumaliza pengine mwaka 2021 tutawasilisha ombi. Sitainunua Arsenal hivi sasa , nitainunua Arsenal nitakapomaliza miradi yote hii kwa sababu najaribu kuinua kampuni hiyo hadi kiwango chengine'', alisema
Na sasa Dangote ameambiwa atakavyogharamika kuinunua klabu hiyo ya Premia na Bob Ratcliffe, ndguye mmoja wa watu matajiri zaidi nchini Uingereza Sir Jim Ratcliffe.
Sir Jim amehusishwa na ununuzi wa klabu ya Chelsea kwa miaka kadhaa sasa, lakini mwezi Agosti uliopita kampuni yake Ineos ilikamilisha makubaliano ya kuinunua klabu ya Nice badala yake.
Nduguye Bob, ambaye ndiye mkuu wa soka katika Ineos amefichua itagharimu fedha ngapi kuinunua klabu ya ligi ya Premia.
Bob aliamnbia gazeti la Financial Times kwamba ununuzi wa klabu sita kuu utagharimu sio chini ya £2bilioni.
Katika ripoti ya Forbes 2020 mfanyabiashara tajiri nchini Nigeria Aliko Dangote ameorodheshwa kwa mara ya tisa mfululizo, kuwa mtu tajiri zaidi barani Afrika .
Dangote mwenye umri wa miaka 62 ambaye anafanya biashara ya Simiti, Sukari na unga wa ngano ana utajiri wa dola Bilioni 10.1.
Wakati huohuo , ununuzi wa timu nyenegine nje ya ligi ya Premia utagharimu kati ya £150m na £350m.
Aliongezea: 'vyote vinauzwa'.