No title



DENI la Taifa katika Mwaka wa Fedha wa 2018/19, limeongezeka kwa asilimia 2.18, kutoka Sh. 50.93 trilioni mwaka 2018 hadi Sh. 53.11 trilioni.

Taarifa hiyo imetolewa leo tarehe 26 Machi 2020 na Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakati akimkabidhi Rais John Magufuli Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu, TAMISEMI, Mashirika ya Umma, Vyama vya Siasa na Sekta binafsi, jijini Dodoma.


Kichere amesema, mchanganuo wa deni hilo ni, deni la ndani Sh 14.86 trilioni, na deni la nje likiwa ni Sh. 38.24 trilioni. Amesema deni hilo ni himilivu.

“Deni la serikali linajumuisha serikali kuu na tassisi zake, hadi kufikia tarehe 30 Juni 2019 ilikuwa trilioni 53.11, la ndani ni 14.86 trilioni., na la nje ni 38.24 trilioni. Ikiwa ongezeko la Sh 2.18 trilioni sawa asilimia 4.Ikilinganishwa na deni la trilioni 50.93 ililoripotiwa tarehe 30 Juni 2018,” amesema Kichere.

 

Kichere amesema sababu za deni hilo kuongezeka ni kushuka kwa thamani ya shilingi na riba ya mikopo halisi.

Kuhusu Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali katika Mwaka wa Fedha 2018/19, Kichere amesema imebaini hati chafu 12, zisizoridhisha 7 na zenye shaka 46, kati ya hati 1082 zilizokaguliwa.

“Katika ukaguzi wa hesabu na mwenendo wa hati za ukaguzi, nilioufanya kwenye taasisi za serikali kuu, serikali za mitaa, vyama vya siasa na mashirika ya umma. Nilikagua hati 1,082 za ukaguzi, kati yake 1017 ni hati zinazoridhisha sawa na 94%, zenye shaka 46 ( 4.25%), zisizoridhisha 7 ( 0.64 %) , hati mbaya 12 (1.11).

Wakati huo huo, Kichere amesema alifanya ukaguzi wa tathimini ya mapendekezo 266 ya ofisi yake kuhusu utekelezwaji wa masuala mbalimbali, na kubaini kwamba mapendekezo 67 hayajaanza kufanyiwa kazi, wakati 95 yako katika utekelezwaji.

Amesema ukaguzi huo umebaini malipo yaliyofanywa taasisi sita kiasi cha 459.2 milioni kwa ajili ya kununua vitu kwa bei juu ya kiwango, ikiwemo Mahakama ya Tanzania iliyotumia Sh. 75 milioni.

Kichere amesema amebaini malipo yaliyofanyikwa bila kudai risiti kaisi cha Sh. 940.92 milioni, zilizolipwa kwa wadhabuni bila kudai risiti kama inavyotakiwa na sheria ya usimamizi wa kodi.

 

Pia, amebaini matumizi yasiyona tija yenye thamani ya 948.3 milioni katika taasisi nne, malipo ya ununuzi na huduma ya vifaa visivyopokelewa vyenye thamani thamani ya Sh. 587.65 milioni katika taasisi 7, kinyume na makubaliano ya mikataba.

“usimamizi wa mapato ya kodi, mwaka wa ulioshia juni 2019 tra ilikusanyw atril 15.74 kati ya makisio tril 18.29 na kutofikia malengo sh tril 2.55 sawa na asilimia 4.”

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad